MAHITAJI:
1. Samaki
2. Chumvi
3. Tangawizi
4. Kitunguu
swaum
5. Limao
6. Pilipili
manga
HATUA YA KWANZ
Unawachukuwa samaki wako kiasi
unaotaka kuwapika unawaparua magamba na kuwatoa utumbo, ukiwamaliza wote
unawaosha na maji safi baada ya kuwaosha unamwaga yale maji ulooshea,
unachukuwa chombo kingine kisicho na maji unawatia wale samaki wako unatia
chumvi kidogo, limao, pilipili manga ilosagwa, tangawizi ilotwangwa na vitunguu
swaum vya kusagwa unavichanganya vyote pamoja na samaki ili kutoa shombo kupata
radha nzuri na harufu nzuri.
HATUA YA PILI:
Baada ya kumaliza kuwaanda samaki
wako unawasha jiko na kutayarisha vitu vya kukaangia samaki mafuta, kikaango,
sahani ya kuwekea samaki, kijiko cha kuepulia kichujio cha kuchujia samaki
baada ya kuwakaanga unawasha jiko unatenga kikaango unaweka mafuta unasubiri
yachemke baada ya kuchemka unatia samaki wako kwa mpangilio ili wasishikane
unawaacha baada ya muda mpka wabadilike rangi na kuwa rangi ya brown
wakishabadilika rangi kuwa wa brown unawatoa unawatia kwenye chujio ili
wajichuje mafuta wakivuja mafuta unawatoa unawaweka kwenye sahani samaki wako
wanakuwa tayari.
Unaweza kuwaandaa kwa kulia ugali,
chips, ndizi za kukaanga au chakula chochote unachoweza kula na samaki wa
kukaanga.