Jumanne, 23 Septemba 2014

CHAPATI ZA KUSUKUMA ZA NAZI



MAHITAJI:
  
1.      Unga wa ngano
2.      Chumvi 
3.      Maji 
4.      Nazi 
5.      Mafuta


HATUA YA KWANZA:

Unandaa unga wako wa ngano kilo 1 unaweka kwenye sinia kubwa kwa ajili ya kuukanda unga huo, ukishauweka kwenye sinia unatia chumvi kidogo unachanganya na unga wakati huo ulisha tengeneza tui la nazi pembeni, unapima tui la nazi  la kwanza  kwenye glasi 1 ya bilauli unamimina kwenye sinia la unga wako unachanganya tui la nazi na unga vikishachanganyika unapima glasi ingine ya maji ya baridi unaweka kwenye unga ulochanganya na tui la nazi unauchanganya unga wote mpaka uchanganyike, ukisha changanyika unaufunika pembeni.

HATUA YA PILI:

Unaandaa vifaa vya kupikia mafuta, frying pan (kikaango), sahani ya kuwekea chapatti, kijiko cha kuepulia, kibao na kisukumio, kisu na unga wa ngano kidogo. Ukishaandaa vitu vya kupikia unachukuwa unga wako ulokwisha ukanda unaukata madonge mawili, kisha unachukuwa kibao cha kuskumia unaweka unga kidongo ili kuzuiya unga uloukanda usinate kwenye kibao, unachukuwa donge moja kati ya yale uloyakata unaliweka kwenye kibao kisha unasukuma kwa muundo wa duara mpaka mpaka linakuwa na unene kiasi kisha unapaka mafuta juu ya unga ulousukuma sehemu yote kisha unanyunyizia unga wa ngano kidogo ili usinatane kisha unalizungusha ukimaliza unachukuwa kisu unakipaka unga kwenye makali ili kisinate kisha unakata vipande vipande saizi ya kati ukimaliza kukata unachukuwa donge moja moja unalikunja muundo wa duara, (kama inavyoonesha kwenye video hapo chini) unachukuwa na donge lingine unalifanya hivyohivyo ukimaliza kukunja zote unaandaa kwa ajili ya kupika unafunika pembeni ili kuandaa mandhari ya kupikia.




 HATUA YA TATU:


Unachukuwa kibao unakipaka unga kidogo kisha unachukuwa donge moja kati ya yale uloyakunjaa unalisukuma kwa duara kuhakikisha duara hilo linakuwa duara lisilopinda isiwe nzito wala nyepesi, unawasha jiko lako unakitenga kikaango juu ya jiko kikipata moto unatia mafuta kidogo hakikisha kikaango chote kina mafuta kasha unayafuta mafuta kwenye kikaango kwa tishu au kitambaa safi, afu unatia chapatti yako hakikisha moto usiwe mkali ukaunguza chapati yako unaangalia kama imebadilika rangi kuwa brown kidogo unaigeuza unatia mafuta kwa chini unakuwa unaigeuzageuza mpaka iwe na rangi ya brown, unageuza na upande wa pili unaweka mafuta unaigeuza mpaka iwe ya brown pia baada ya hapo unaitoa unaiweka kwenye sahani unachukuwa donge linguine unafanya kama ya mwanzompaka umalize zote.






 Chapati unaweza kulia na rost ya maini au nyama yoyote, maharage ya nazi hata ya mawese au chai ya maziwa na chai ya rangi na kwa muda wowote.










Hakuna maoni:

Chapisha Maoni