Jumatatu, 29 Septemba 2014

SAMAKI WA KUKAANGA (VIBUA)




MAHITAJI:

1.      Samaki 
2.      Chumvi 
3.      Tangawizi 
4.      Kitunguu swaum 
5.      Limao 
6.      Pilipili manga




HATUA YA KWANZ

Unawachukuwa samaki wako kiasi unaotaka kuwapika unawaparua magamba na kuwatoa utumbo, ukiwamaliza wote unawaosha na maji safi baada ya kuwaosha unamwaga yale maji ulooshea, unachukuwa chombo kingine kisicho na maji unawatia wale samaki wako unatia chumvi kidogo, limao, pilipili manga ilosagwa, tangawizi ilotwangwa na vitunguu swaum vya kusagwa unavichanganya vyote pamoja na samaki ili kutoa shombo kupata radha nzuri na harufu nzuri.






 HATUA YA PILI:

Baada ya kumaliza kuwaanda samaki wako unawasha jiko na kutayarisha vitu vya kukaangia samaki mafuta, kikaango, sahani ya kuwekea samaki, kijiko cha kuepulia kichujio cha kuchujia samaki baada ya kuwakaanga unawasha jiko unatenga kikaango unaweka mafuta unasubiri yachemke baada ya kuchemka unatia samaki wako kwa mpangilio ili wasishikane unawaacha baada ya muda mpka wabadilike rangi na kuwa rangi ya brown wakishabadilika rangi kuwa wa brown unawatoa unawatia kwenye chujio ili wajichuje mafuta wakivuja mafuta unawatoa unawaweka kwenye sahani samaki wako wanakuwa tayari.




 Unaweza kuwaandaa kwa kulia ugali, chips, ndizi za kukaanga au chakula chochote unachoweza kula na samaki wa kukaanga. 












Maoni 2 :

  1. safi sana inapendeza hatimaye nimejua

    JibuFuta
  2. Hahahahaaaa karbu tena bro na kama kuna kitu unataka kujua unaniambia tu ni chakula gani unataka nikupikie na mie ntafanya hvyo usjali @all mwanguku

    JibuFuta