Jumatano, 1 Oktoba 2014

PIZZA YA SOSEJI




                 MAHITAJI:



1.      Unga wa ngano
2.      Soseji
3.      Nyanya
4.      Karoti
5.      Hoho
6.      Chumvi
7.      Njegere
8.      Blue band
9.      Hamira
10.  Sukari
11.  Pizza sauce
12. 



 HATUA YA KWANZA:


Unakanda unga wa ngano kilo 1 na blue band kidogo, hamira, sukari, na chumvi kiasi unakanda kama unga wa chapati ukishakuwa sawa unakata madonge kulingana na unga ulokanda kisha unafunika kwa dakika 5 zikiisha dakika 5 unachukuwa donge lako unasukuma kama unavyosukuma chapati.


HATUA YA PILI:


Unaichukuwa ile chapatti uliosukuma unaipaka pizza souce kwa juu baada ya hapo unaweka soseji ambayo ulisha isaga na mashine unachukuwa njegere ambazo zimesha chemshwa, hoho, karoti na nyanya unavipanga vizuri juu ya ile chapatti ulioisukuma baada ya hapo unaweka chizz souce ukimaliza kuweka chizz souce unaiweka kwenye oven kwa muda wa dakika 15 hakikisha moto uwe kiasi ili isiungue au kukaauka.











Pizza yetu inakuwa tayari unaweza kulia juice, soda, hata chai.


















Hakuna maoni:

Chapisha Maoni