Ijumaa, 24 Oktoba 2014

NDIZI ZA SUKARI

MAHITAJI

1. Ndizi
2. Nazi
3. Sukari
4. Hiliki

HATUA YA KWANZA:

 Unachukuwa ndizi za sukari unazimenya maganda ukishamaliza unachukuwa sufuria utakayo pikia, unachagua katika yale maganda ulomenya ambayo mazuri hayajachoka jama maganda 2 au 3 unayaosha vizuri kwa maji safi kisha unayatandaza kwenye sufuria utakayo pikia.




 HATUA YA PILI:

 Unazichukuwa ndizi zako unaziosha vizuri kisha unaziweka kwenye lile sufuria uliloweka maganda chini ya kupikia kisha unanyunyizia sukari kidogo kulingana na ndizi zako. Unachukuwa nazi unakuna kulingana na wingi wa ndizi baada ya kuikuna unachuja unatoa matui 2 tui la 1 ni lile zito na tui la 2 ni jepesi basi ubachukuwa tui la 2 unamimina kwenye sufuria ndio utakayo tengea bila kuweka maji yoyote baada ya hapo unatenga jikoni unaacha zinachemka mpaka maji yapunguwe yakipunguwa unatia tui la 1 usifunike unakuwa unavuruga taratibu ili zisikatike mpka lile tui la 1 lichemke kisha unaziacha zichemke zenyewe kisha unaangalia kama zimebakia na urojourojo unaziepua.












Ndizi zinakuwa tayari kwa kuliwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni