Jumamosi, 25 Oktoba 2014

WALI WA PILAU WA NYAMA YA NG'OMBE

MAHITAJI:

1. Mchele
2. Nyama ya ng'ombe
3. Viazi mviringo
4. Vitunguu maji
5. Nyanya
6. Mdalasini
7. Chumvi
8. Mafuta
9. Viungo vya pilau (mchanganyiko)
10. Sukari




 HATUA YA KWANZA:

Unachambua mchele wako kilo 1 au kiasi chochote unachotaka kupika unachemsha nyama yako utakayo changanya kwenye pilau yako ukiwa umewrka vhumvi, tangawizi, na vitunguu swaum utamenya viazi mviringo vyako utaanda viungo vya pilau vilivyo sagwa ukimaliza utaangalia kama nyama yako imeiva utaipua na kuandaa mchele wako kwa kuuchagua kwa ajili ya kuanza kupikautaosha mchele wako mara 2 kwa maji safi.


HATUA YA PILI:

Utawasha jiko lako utatenga sufuria utakayo pikia pilau yako hakikisha sufuria linatosha mchele ulopima au kupanga kupika utaweka mafuta kiasi utaacha yapate moto kiasi yakishapata moto utaweka vitunguu majivikibadilika rangi na kuwa ya brown utatia vitunguu swaum vilivyosagwa utachanganya vizuri baada ya hapo utaweka viungo vya pilau vilivyo changanywa unavichanganya na vitunguu swaum vikikaangika unaweka nyamaunaikaanga nayo mpaka ichanganyike na viungo kisha unaweka maji kiasi cha mchele utakao pika unaweka chumvi kiasi na sukari kiasi cha kijiko 1 cha kulia chakula kwa ajili ya kutoa gesi ya viungo unafunika unasubiria maji yachemke yakisha chemka unatia mchele wako unageuzageuza ili mchele uchanganyike na viungo, ukishachanganyika unafunika kusubiria maji yakauke.











 HATUA YA TATU:

Unachukuwa viazi mviringo unavikaanga kidogo kwenye mafuta ya moto kiasi kama dakika 4 kisha unavitoa ili vivuje mafuta baada ya hapo unafunua sufuria lako la wali kama maji yamekauka kisha unaweka viazi mviringo ulivyo vikaanga kisha unageuza kuvichanganya na wali unafunika kisha unapunguza moto unaweka juu na chini unakaa baada ya muda unafunua kuugeuza kuuangalia kama umeiva unaepua.





  Pilau yako inakuwa tayari imeiva na kuliwa.

Maoni 3 :

  1. Hongera bibie, tujuze tupikie familia na furaha izidi, nakuaminia!

    JibuFuta
  2. Asante sana kwa kuchangia kuongeza ujuzi .

    Nimeipenda recipe yako. Nimejifunza mengi hasa katika mlolongo kuanzia kukaanga viungo, kufuatia kukaanga nyama na viungo na kisha kuongeza maji kuupika mseto kufikia pilau murua. Na pale upoongeza sukari kupunguza gesi kwenye pilau.

    Napenda kuongezea kwa wale wanaotumia rice cooker baada ya mseto kuwa tayari unaweza kuhamishia kwenye Jiko hilo nakupika mpaka iive.

    JibuFuta
  3. Shukran naimani mtajifunza vingi na kuongeza ujuzi wa vyakula mbalimbali kupitia blog hii @Nuru kalufya

    JibuFuta