Jumanne, 7 Oktoba 2014

JUICE YA TIKITI NA PASION




MAHITAJI:

1.      Tikiti 
2.      Pasion 
3.      Sukari 
4.      Maji









HATUA YA KWANZA:


Unachukuwa tikiti lako unaliosha na maji masafi baada ya hapo unalikata vipande vidogovidogo  unaweka pembeni, unachukuwa pia mapasion inayaosha vizuri na maji safi unakata katikati unatoa mbego za ndani kwa kutumia kijiko  unaweka pembeni.



HATUA YA PILI:


Unaanda vifaa utakavyotumia kutengenezea juice yako Brenda na jagi lake, mabakuli 2, chujio, maji, kijiko, jagi na sukari ukimaliza unachota matikiti kiasi unaweka kwenye brenda unachota na kijiko tena mapasion unaweka kwenye brenda baada ya hapo unaweka maji kidogo afu unasaga ikishasagika unazima brenda unamimina kwenye bakuli moja baada ya hapo unachukuwa chujio unaweka kwenye bakuli linguine unachuja baada ya kuchuja unaiweka juice yako kwenye jagi afu unaweka kwenye fridge ili iate baridi.











Juice yako inakuwa tayari kwa kunywa mie leo nimeandaa kwa ajili ya chakula cha mchana.

























Hakuna maoni:

Chapisha Maoni