Ijumaa, 3 Oktoba 2014

MAANDAZI YA KUOKA (MABANZI)





MAHITAJI:

1.      Unga wa ngano 
2.      Blue band 
3.      Hamira 
4.      Maziwa 
5.      Mayai 
6.      Sukari 
7.      Chumvi


HATUA YA KWANZA


Unaandaa unga wako wa ngano kiasi unacho taka kupika unaweka kwenye sinia au chombo kipana kasha unaweka unga wako unachanganya na blue band, sukari kidogo, chumvi kidogo, hamira na mayai 2 kulingana na unga wako kasha unatia maziwa glass 2 afu unaukanda unga ule mpaka ulainike na kuchanganyikana vitu vyote ulivyoweka. Baada ya hapo unakatakata madonge kasha unafunika pembeni unayaacha yaumuke kwa muda wa dakika 5.




  HATUA YA PILI:


Unachukuwa donge moja unasukuma kama mfano wa chapati lakini lakini yenyewe yanakuwa manene kiasi ukimaliza unakata kwa muundo wowote unaoutaka kama duara, pembe nne au pembe tatu utakavyopenda mwenyewe ukimaliza kukata unachukuwa trey lako la oven unapaka blue band kidogo kwa kusambaza sehem zote za trey ili ukiweka maandazi yako yasishike ukimaliza unachukuwa maandazi yako uloyakata unayapanga vizuri kwenye trey uloipaka blue band afu unayaacha kwa muda wa dakika 3 kisha unayaweka kwenye oven (kuoka) unaweka moto mdogomdogo ili yasikauke na kuunguwa unahakikisha moto wa chini na wa juu upo sawa unakaa muda wa dakika 15 unaangalia kama yamebalika rangi nakuwa ya rangi ya brown kiasi kasha unatoa. 





Maandazi au mabanzi yako yanakuwa tayari kwa kula unaweza kula kwa wakati wowote kutumia chai, juice, maziwa hata mboga yoyote.













Hakuna maoni:

Chapisha Maoni