MAHITAJI:
1. Unga
wa ngano
2. Maziwa
3. Blue
band
4. Hamira
5. Ufuta
6. Nyama
7. Ute
wa yai (mayai)
8. Vitunguu
9. Nyanya
10. Kabeji
11. Hoho
12. Karoti
13. Chumvi
14. Mayonnaise
15. Kotmir
16. Kitunguu
swaum
17. Tangawizi
HATUA YA KWANZA:
Unachukuwa unga wa ngano kiasi unachotaka kupika kwa
siku hiyo unauweka kwenye chombo kipana au sinia safi unatia maziwa glasi 2,
hamira, blue band, chumvi afu unakanda kama unavyokanda unga wa chapatti ukishamaliza
unatengeneza madonge mazuri yanayo lingana afu unayapaka juu ute wa yai ili
unapoweka ufuta usiweze kutoka baada ya hapo unanyunyizia ufuta juu ukimaliza
unayaweka pembeni kwa muda wa dakika 5 ili yaumuke, afu unayaweka kwenye oveni
kwa muda wa dakika 15 mpaka yawe ya brown baada ya hapo unayatoa.
HATUA YA PILI:
Unachukuwa zile skonzi unazikata katikati na kisu
kikali na kisafi kasha unaanda nyama ilokwisha chemshwa ikiwa imetiwa chumvi
kidogo, kotmir, tangawizi na vitunguu swaum na imeshasagwa kasha unaandaa mayai
yalochemshwa unayakata kwa muundo wa duara, hoho, karoti, nyanya, vitunguu maji
na kabeji vyote unavikata kwa muundo wa viduara vidogo vidogo nay a kupendeza.
HATUA YA TATU:
Unachukuwa skonzi ilokatwa katikati unaipaka
mayonnaise kasha unaweka nyama ilosagwa afu unatia chizz ya siles unaweka
nyanya ulokata, vitunguu maji, mayai, hoho, karoti na kabeji afu unaweka
mayonnaise juu kisha unachukuwa kipande cha juu unafunika.
Bagger yako inakuwa tayari.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni