MAHITAJI:
1 Ndizi
malindi
2. Chumvi
3. Hoho
4. Karoti
5. Maji
6. Kitunguu
7. Nazi
HATUA YA KWANZA:
Unachukuwa ndizi
malindi zako kiasi ulicho panga kupika unazimenya maganda kasha unaziweka
kwenye chombo chenye maji masafi unaziosha mara mbili, chukuwa sufuria yako
unayotaka kupikia zipange vizuri ndizi zako kwenye hiyo sufuria kwa mapishi
yake hazitakiwi kukatwa unazipika hivyohivyo nzimanzima, zitenge jikoni ndizi
zako weka maji kidogokulingana na kipimo cha ndizi ulizo pika funika na mfuniko
vizuri hakikisha mvuke hautoki.
HATUA YA PILI:
Baada ya muda kidogo angalia kama maji uloweka
yamepunguwa unakatia karoti, hoho na kitunguu afu unafunika kwa muda kidogo
chumvi utaweka ukiwa unaweka tui la nazi, andaa nazi yako moja kuna ukimaliza chuja tui lako
la naziya kwanza lile zito ukimaliza
weka tui lako la nazi kwenye ndizi kwa ajili ya kupata radha harufu nzuri na
muonekano mzuri wa chakula changanya nazi yako na nazi mpaka tui lichemke ili
lisikatike utapunguza moto kidogo utaacha lichemke mpka ubakie uji uji utaepua.
Ndizi zita kuwa tayari zimeiva unaweza kula kwa
samaki wa kukaanga au nyama.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni