Jumamosi, 25 Oktoba 2014

WALI WA PILAU WA NYAMA YA NG'OMBE

MAHITAJI:

1. Mchele
2. Nyama ya ng'ombe
3. Viazi mviringo
4. Vitunguu maji
5. Nyanya
6. Mdalasini
7. Chumvi
8. Mafuta
9. Viungo vya pilau (mchanganyiko)
10. Sukari




 HATUA YA KWANZA:

Unachambua mchele wako kilo 1 au kiasi chochote unachotaka kupika unachemsha nyama yako utakayo changanya kwenye pilau yako ukiwa umewrka vhumvi, tangawizi, na vitunguu swaum utamenya viazi mviringo vyako utaanda viungo vya pilau vilivyo sagwa ukimaliza utaangalia kama nyama yako imeiva utaipua na kuandaa mchele wako kwa kuuchagua kwa ajili ya kuanza kupikautaosha mchele wako mara 2 kwa maji safi.


HATUA YA PILI:

Utawasha jiko lako utatenga sufuria utakayo pikia pilau yako hakikisha sufuria linatosha mchele ulopima au kupanga kupika utaweka mafuta kiasi utaacha yapate moto kiasi yakishapata moto utaweka vitunguu majivikibadilika rangi na kuwa ya brown utatia vitunguu swaum vilivyosagwa utachanganya vizuri baada ya hapo utaweka viungo vya pilau vilivyo changanywa unavichanganya na vitunguu swaum vikikaangika unaweka nyamaunaikaanga nayo mpaka ichanganyike na viungo kisha unaweka maji kiasi cha mchele utakao pika unaweka chumvi kiasi na sukari kiasi cha kijiko 1 cha kulia chakula kwa ajili ya kutoa gesi ya viungo unafunika unasubiria maji yachemke yakisha chemka unatia mchele wako unageuzageuza ili mchele uchanganyike na viungo, ukishachanganyika unafunika kusubiria maji yakauke.











 HATUA YA TATU:

Unachukuwa viazi mviringo unavikaanga kidogo kwenye mafuta ya moto kiasi kama dakika 4 kisha unavitoa ili vivuje mafuta baada ya hapo unafunua sufuria lako la wali kama maji yamekauka kisha unaweka viazi mviringo ulivyo vikaanga kisha unageuza kuvichanganya na wali unafunika kisha unapunguza moto unaweka juu na chini unakaa baada ya muda unafunua kuugeuza kuuangalia kama umeiva unaepua.





  Pilau yako inakuwa tayari imeiva na kuliwa.

Ijumaa, 24 Oktoba 2014

NDIZI ZA SUKARI

MAHITAJI

1. Ndizi
2. Nazi
3. Sukari
4. Hiliki

HATUA YA KWANZA:

 Unachukuwa ndizi za sukari unazimenya maganda ukishamaliza unachukuwa sufuria utakayo pikia, unachagua katika yale maganda ulomenya ambayo mazuri hayajachoka jama maganda 2 au 3 unayaosha vizuri kwa maji safi kisha unayatandaza kwenye sufuria utakayo pikia.




 HATUA YA PILI:

 Unazichukuwa ndizi zako unaziosha vizuri kisha unaziweka kwenye lile sufuria uliloweka maganda chini ya kupikia kisha unanyunyizia sukari kidogo kulingana na ndizi zako. Unachukuwa nazi unakuna kulingana na wingi wa ndizi baada ya kuikuna unachuja unatoa matui 2 tui la 1 ni lile zito na tui la 2 ni jepesi basi ubachukuwa tui la 2 unamimina kwenye sufuria ndio utakayo tengea bila kuweka maji yoyote baada ya hapo unatenga jikoni unaacha zinachemka mpaka maji yapunguwe yakipunguwa unatia tui la 1 usifunike unakuwa unavuruga taratibu ili zisikatike mpka lile tui la 1 lichemke kisha unaziacha zichemke zenyewe kisha unaangalia kama zimebakia na urojourojo unaziepua.












Ndizi zinakuwa tayari kwa kuliwa.

Jumatatu, 20 Oktoba 2014

Sababu za kuvunjika kwa ndoa

Mapishi ni nguzo kubwa sana katika ndoa. Swala hili limekua tatizo kubwa katika karne hii, sababu zimekua nyingi sana. Ungana nami nikiwa  na wataalamu Bi.  Anasra Kihanza na Mwatum Konzanga kupata ufumbuzi zaidi.


Sababu za kuvunjika kwa ndoa

Jumanne, 7 Oktoba 2014

JUICE YA TIKITI NA PASION




MAHITAJI:

1.      Tikiti 
2.      Pasion 
3.      Sukari 
4.      Maji









HATUA YA KWANZA:


Unachukuwa tikiti lako unaliosha na maji masafi baada ya hapo unalikata vipande vidogovidogo  unaweka pembeni, unachukuwa pia mapasion inayaosha vizuri na maji safi unakata katikati unatoa mbego za ndani kwa kutumia kijiko  unaweka pembeni.



HATUA YA PILI:


Unaanda vifaa utakavyotumia kutengenezea juice yako Brenda na jagi lake, mabakuli 2, chujio, maji, kijiko, jagi na sukari ukimaliza unachota matikiti kiasi unaweka kwenye brenda unachota na kijiko tena mapasion unaweka kwenye brenda baada ya hapo unaweka maji kidogo afu unasaga ikishasagika unazima brenda unamimina kwenye bakuli moja baada ya hapo unachukuwa chujio unaweka kwenye bakuli linguine unachuja baada ya kuchuja unaiweka juice yako kwenye jagi afu unaweka kwenye fridge ili iate baridi.











Juice yako inakuwa tayari kwa kunywa mie leo nimeandaa kwa ajili ya chakula cha mchana.

























Jumatatu, 6 Oktoba 2014

BUGGER



MAHITAJI:

1.      Unga wa ngano 
2.      Maziwa 
3.      Blue band 
4.      Hamira 
5.      Ufuta 
6.      Nyama 
7.      Ute wa yai (mayai) 
8.      Vitunguu 
9.      Nyanya 
10.  Kabeji 
11.  Hoho 
12.  Karoti 
13.  Chumvi 
14.  Mayonnaise 
15.  Kotmir 
16.  Kitunguu swaum 
17.  Tangawizi

HATUA YA KWANZA:

Unachukuwa unga wa ngano kiasi unachotaka kupika kwa siku hiyo unauweka kwenye chombo kipana au sinia safi unatia maziwa glasi 2, hamira, blue band, chumvi afu unakanda kama unavyokanda unga wa chapatti ukishamaliza unatengeneza madonge mazuri yanayo lingana afu unayapaka juu ute wa yai ili unapoweka ufuta usiweze kutoka baada ya hapo unanyunyizia ufuta juu ukimaliza unayaweka pembeni kwa muda wa dakika 5 ili yaumuke, afu unayaweka kwenye oveni kwa muda wa dakika 15 mpaka yawe ya brown baada ya hapo unayatoa.








 HATUA YA PILI:

Unachukuwa zile skonzi unazikata katikati na kisu kikali na kisafi kasha unaanda nyama ilokwisha chemshwa ikiwa imetiwa chumvi kidogo, kotmir, tangawizi na vitunguu swaum na imeshasagwa kasha unaandaa mayai yalochemshwa unayakata kwa muundo wa duara, hoho, karoti, nyanya, vitunguu maji na kabeji vyote unavikata kwa muundo wa viduara vidogo vidogo nay a kupendeza.





 HATUA YA TATU:

Unachukuwa skonzi ilokatwa katikati unaipaka mayonnaise kasha unaweka nyama ilosagwa afu unatia chizz ya siles unaweka nyanya ulokata, vitunguu maji, mayai, hoho, karoti na kabeji afu unaweka mayonnaise juu kisha unachukuwa kipande cha juu unafunika.







Bagger yako inakuwa tayari.